BLOGGER LINK

https://www.blogger.com/rearrange?blogID=5997489750482377630§ionId=crosscol&action=editWidget&widgetType=HTML&referrer=directory

Monday, August 26, 2019

YANGA NEWS...

Imeelezwa kuwa ushindi wa Yanga nchini Botswana ulichangiwa na mambo mengi, ikiwamo kitendo cha Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela kuwazidi ujanja wenyeji wao.
Mmoja wa Watanzania wanaoishi Botswana, Dickson John, aliliambia gazeti la Bingwa kuwa viongozi wa Township Rollers walitishwa na kocha wao, Tomas Trucha, raia wa Jamhuri ya Czech alipowaambia Yanga si timu ya mchezo mchezo hivyo kusuka mikakati kabambe ya nje ya uwanja ili kuwamaliza Wanajangwani hao.
"Walipanga kuwaanza kuwadhibiti Yanga toka uwanja wa ndege hadi hotelini, waliposikia kuna viongozi wa Yanga walishatangulia hapa, walipagawa, wakahofu mambo yao yasijejulikana na kujitia aibu CAF (Shirikisho la Soka Afrika), matokeo yake wakaamua kusubiri matokeo ya uwanjani," alisema.
Watanzania waishio Botswana walikuwa na mchango mkubwa kwani walihaha kushirikiana na Mwakalebela na viongozi wengine wa Yanga kuhakikisha hakuna hujuma yoyote inayofanyiwa timu yao na mwisho wa siku, mshindi apatikane uwanjani kama ilivyokuwa.
"Jana (juzi) baada ya mchezo, viongozi wa Rollers na mashabiki wao, walichanganyikiwa, hawakuamini kilichotokea," alisema John.
Yanga haikumpeleka Mwakalebela Botswana kwa bahati mbaya, uzoefu wake kwenye masuala ya Kimataifa kufahamiana na watu nchini Botswana ilikuwa ni faidi kubwa kwa Yanga

No comments:

Post a Comment

ahsante